IQNA

Mashindano ya kila mwaka ya Qur'ani kufanyika Bahrain

18:21 - January 18, 2011
Habari ID: 2067020
Mashindano ya kila mwaka ya masomo ya Qur'ani ya Jumuiya ya ad-Dhikrul Hakim yamepangwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu nchini Bahrain.
Mashindano hayo yamepangwa kufanyika katika hatua saba za usomaji na sauti nzuri ya Qur'ani, hifdhi, tafsiri, utafiti wa Qur'ani, uchoraji na hati ya Qur'ani, kaligrafia ya Qur'ani na upigaji picha. Jumuiya iliyotajwa imesema kuwa lengo la kufanyika mashindano hayo ni kueneza utamaduni wa Qur'ani na kulea kizazi cha Qur'ani kinachoeneza ujumbe wa kitabu hicho kitakatifu.
Imesema kuwa watu walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kufanya hivyo katika zaidi ya kitengo kimoja cha mashindano hayo.
Usajili wa majina ya washiriki ulianza siku ya Jumapili tarehe 16 na utaendelea hadi tarehe 5 Februari. 732986
captcha