Akizungumza katika sherehe hiyo, Anwaar as-Sweiri, mwanafikra wa Saudi Arabia amesema kuwa wanafunzi wa India na Pakistan ambao lugha yao si ya Kiarabu na ambao licha ya kuhifadhi wanatakiwa pia kufahamu maana ya aya wanazohifadhi, wamefanya vizuri zaidi kuwaliko wanafunzi wa Saudi Arabia.
Makumi ya wanafunzi wamefanikiwa kuhitimu hifhi ya Qur'ani nzima katika shule hiyo iliyoanzishwa miaka mitatu iliyopita.
Kuna wanafunzi 60 wanaofuatilia masomo ya hifdhi ya Qur'ani katika shule hiyo hivi sasa. Sherehe hiyo ilimalizika kwa wanafunzi waliohifadhi Qur'ani nzima kutunukiwa zawadi. 733511