IQNA

Khatibu wa sala ya Ijumaa Tehran asema haki haiwezi kuzimika

11:27 - January 22, 2011
Habari ID: 2068180
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran katika hotuba yake ya pili ameashiria baadhi ya njama zinazofanywa dhidi ya Uislamu na vilevile matuko ya Tunisia na kusimama kidete watu wa nchi hiyo mbele ya udikteta na kusema : “Historia imeonyesha kuwa harakati katika mkondo wa haki haiwezi kuzimwa”
Akihutubia maelfu ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Emami Kashani amesema kuwa, nchi za Magharibi zinapaswa kuangalia matukio yaliyopita sambamba na kuchukua ibra na funzo kutoka katika matukio ya huko nyuma na kutorejea kufanya makosa katika duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5 + 1, nchini Uturuki. Ayatullah Kashani amezungumzia suala la kuanza duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia kati ya pande hizo mbili mjini Istanbul Uturuki na kuongeza kuwa, nchi za Magharibi zinapaswa kuweka pembeni misimamo yao isiyo ya kimantiki.
Huku akisisitiza kuwa miradi ya nyuklia ya Iran inafanyika kwa malengo kuzalisha nishati na masuala za kielimu, Ayatullah Kashani ameongeza kuwa, hivi karibuni wawakilishi kutoka nchi 120 duniani walipata fursa ya kukagua na kutembelea taasisi za nyuklia za Iran huko Arak na Natanz na wamethibitisha kwamba shughuli za nyuklia za hapa nchini zinafanyika kwa uwazi kabisa na tena kwa malengo ya amani.
Ayatullah Kashani ameongeza kuwa, mashinikizo yanayotolewa na madola ya Magharibi hayataweza kuwavunja moyo wananchi wa Iran.
Kwenye sehemu nyingine ya khutba ya pili ya sala ya Ijumaa mjini Tehran, Ayatullah Kashani ameitaka serikali ya Jamhuri ya Azerbaijan kusikiliza matakwa ya wananchi wa nchi hiyo na ametaka ifutwe marufuku ya uvaaji wa hijabu mashuleni.
734209
captcha