IQNA

Mkutano wa kimataifa wa kuwahami mateka wa Kipalestina Moroco

20:23 - January 22, 2011
Habari ID: 2068784
Mkutano wa kimataifa wa kuwahami mateka wa Palestina ulianza jana Ijumaa katika mji mkuu wa Moroco Rabat.
Tovuti ya "map.ma" imeripoti kuwa mkutano huo ambao utamalizika kesho unahudhuriwa na wanaharakati wa haki za binadamu, wanadiplomasia wa nchi za kigeni, wanasiasa na wasanii.
Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na suala la kuundwa muungano wa kimataifa wa haki za binadamu kwa ajili ya kuwatetea mateka wa Kipalesina katika jela za utawala ghasibu wa Israel.
Mkutano huo unafanyika chini ya anwani ya "Kukomboa Mateka wa Kipalestina, Wajibu wa Kimataifa. 734529
captcha