Kesi za Masjid Nur, msikiti wa Waislamu Masuni na Masjid Qanati, Msikiti wa Waislamu Mashia mjini New Delhi zilijadiliwa katika kikao kilichohudhuriwa na Mkuu wa Masuala ya Utamaduni wa Wilaya ya Uttar Pradesh.
Misikiti hiyo ilirejeshewa jamii za Waislamu kufuatia malalamiko ya Mahakama Kuu ya India.
Jalal Haidar Naqavi mkuu wa Majlis Ulama Islam amesema, “tukio hilo limeonyesha kuwa matatizo yote yawe ya kisiasa, kijamii au kiuchumi yanaweza kutatuliwa kwa kudumisha umoja wetu”.
Amepongeza juhudi za Haj Sho’aib Iqbal, Asif Mohammad Khan na Seyyed Ahmad Bukhari, Imam wa Msikiti Mkuu wa New Delhi katika kadhia hiyo.
734356