Kwa mujibu wa tovuti ya LA Jamaat, katika wiki hii ratiba mbalimbali za maombolezo zinafanyika katika kituo hicho. Miongoni mwa ratiba hizo ni hotuba zinazotolewa na shakhsia pamoja na wanazuoni wa Kiislamu kwa ajili ya kuhuisha maombolezo hayo muhimu katika historia ya Kiislamu.
Mbali na hutuba kuhusiana na shakhsia na mapambano ya Imam Hussein (as) mbele ya watawala dhalimu wa Banu Ummayya, vikao vya usomaji na tafsiri ya Qur'ani pamoja na dua ni miongoni mwa ratiba zitakazotekelezwa katika kituo hicho cha Kiislamu nchini Marekani.
Ratiba hizo zinatazamiwa kumalizika hapo kesho Jumanne ambayo ni siku ya Arbaini ya Imam Hussein (as). 735612