Tovuti ya “alukah.net” imeripoti kuwa mkutano huo ulifanyika jana kwa usimamizi wa Jumuiya ya Kupambana na Uzushi ya Marekani kwa ushirikiano wa ofisi ya msemaji wa Kiislamu wa jimbo la Georgia. Mkutano huo umehudhuriwa na shakhsia na wasomi kadhaa wa Marekani.
Moja ya malengo ya mkutano huo limetajwa kuwa ni kujibu ufahamu usiokuwa sahihi wa wasiokuwa Waislamu kuhusu mafundisho ya dini hiyo na Qur’ani Tukufu. Vilevile washiriki wa mkutano huo walijadili sheria za Qur’ani Tukufu na jinsi ya kuamiliana na wasiokuwa Waislamu na pia nafasi ya mwanamke na familia katika jamii.
Baadhi ya waliohutubia mkutano huo wamezungumzia nafasi ya Qur’ani katika kuongoza maisha ya Waislamu. 737536