Akizungumzia suala hilo, Ibrahim Mansi, mkuu wa uhusiano wa umma wa kitengo cha habari cha Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Hifdhi ya Qur'ani ya mkoa uliotajwa amesema kuwa masomo hayo yatakayochukua muda wa wiki moja yatajumuisha masomo ya malezi, warsha za mafunzo na masomo ya kitaalamu kwa lengo la kunyanyua kiwango cha elimu na uzoefu wa walimu wa Qur'ani.
Ameendelea kusema kuwa lengo la kufanyika masomo hayo ya kila mwaka ni kuanishwa viwango na sifa za mwalimu bora wa Qur'ani. Amesema Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Hifdhi ya Qur'ani ya Jeddah nchini Saudi Arabia huandaa kila mwaka masomo tofauti maalumu ya kunyanyua uzoefu na ujuzi wa walimu wa Qur'ani. 737887