IQNA

Maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kufanyika Ghana

13:38 - January 30, 2011
Habari ID: 2072138
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Ghana kimeandaa Tamasha ya Fajr.
Abbasali Afsari mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Ghana amemualika Waziri wa Utamaduni wa Ghana Alexander Asum-Ahensah kushiriki katika sherehe za ufunguzi wa tamasha hiyo.
Katika mkutano wake na Asum-Ahensah, afisa huyo wa Iran amempongeza kwa mnasaba wa mwaka mpya na kupongeza hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Utamaduni ya Ghana katika kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Accra.
Kwa upande wake Asum-Ahensah amesema wizara yake iko tayari kushirikiana katika kuandaa tamasha ya Fajr.
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyoongozwa na hayati Imam Khomeini MA yalipata ushindi Februari 11, 1979. Kila mwaka sherehe za kuadhimisha ushindi huo hufanyika Iran na kote duniani.
737587
captcha