Kwa mujibu wa tovuti ya Times Alive duru hiyo ya mashindano itafanyika mjini Pretoria. Washiriki wa mashindano hayo wanatazamiwa kuchuana katika Msikiti wa Westville katika mkoa wa Kwazulu Natal tarehe 26 Februari.
Washindi wa hatua hiyo ya mashindano watapata fursa ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya hifdhi ya Qur'ani yanayotazamiwa kufanyika baadaye nchini Saudi Arabia.
Taasisi ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu ya Afrika Kusini ambayo ndiyo inayoaandaa mashindano hayo imezitaka shule zote za Kiislamu za nchi hiyo kuandikisha majina ya wanafunzi walio na hamu ya kushiriki kwenye mashindano hayo kufikia tarehe 10 Februari.
Mashindano hayo ya kila mwaka yana lengo la kuwashajiisha vijana wa Afrika Kusini kuzingatia na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. 738728