IQNA

Qur'ani yapotoshwa katika nchi kubwa zaidi ya Kiislamu

18:32 - January 31, 2011
Habari ID: 2073490
Kanali ya televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa asilimia 90 na nakala za kitabu kitukufu cha Qur'ani katika nchi kubwa zaidi ya Kiislamu yaani Indonesia, zinachapishwa na taasisi za uchapishaji zisizokuwa za Kiislamu, suala ambalo linasababisha makosa ya kichapa.
Adang Kartana ambaye ni mkurugenzi wa moja ya taasisi za uchapishaji Qur'ani nchini Indonesia amesema kazi ya uchapishaji nakala za Qur'ani katika taasisi hizo haifanyiki kwa uangalifu na ukusanyaji na ugawaji wa nakana hizo hauzingatii nafasi na heshima ya kitabu hicho kitukufu.
Ameongeza kuwa baadhi ya nakala zlizochapishwa katika taasisi hizo za uchapishaji zina makosa na Waislamu na taasisi za kidini zimekuwa zikizirejesha kwa wachapishaji wake baada ya kugundua makosa hayo ambao amesema yanafanyika kwa makusidi. Hata hivyo wamiliki wa taasisi hizo za uchapishaji wanakanusha kwamba makosa hayo yanaanyika kwa makusudi.
Adang Kartana amesisitiza juu ya kuzidishwa udhibiti na usimamizi wa kazi ya uchapishaji wa nakala za Qur'ani Tukufu nchini Indonesia. Amesema baadhi ya taasisi hizo za uchapishaji zinachapisha Qur'ani kwa kutumia karatasi duni na zisizokuwa na viwango kwa shabaha ya kupata faida zaidi, jambo ambalo linakivunjia heshima Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu. 739638

captcha