IQNA

Sherehe ya kuwaenzi mahafidhi wa kike zafanyika Palestina

11:58 - February 03, 2011
Habari ID: 2074613
Sherehe ya kuwaenzi mahafidhi wa kike wa Qur'ani imefanyika katika Kituo cha Kuhifadhisha na Tajwidi ya Qur'ani Tukufu katika eneo la Salfit katika eneo la Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan huko Palestina.
Sherehe hiyo imesimamiwa na Kamati ya Masuala ya Dini ya eneo la Salfit katika Msikiti wa al Hauqala. Wanawake 43 wa Kipalestina waliofanikiwa kukamilisha masomo ya kuhifadhi na tajwidi ya Qur'ani wameenziwa katika sherehe hiyo.
Gavana wa eneo hilo Abdul Sattar Auda amehutubia sherehe hiyo akiwashukuru watu wote waliofanikisha masomo hayo. Amesema vituo vingi vya masomo ya Qur'ani vimeanzishwa katika eneo la Salfit.
Amewataka pia kina mama walishiriki katika masomo hao kuwahamasisha watoto wao kushiriki katika vituo vya Qur'ani. Mwishoni mwa sherehe hiyo kina mama waliohitimu masomo ya Qur'ani katika kituo hicho walitunukiwa zawadi. 740752

captcha