IQNA

Kongamano la kimataifa la kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu kufanyika Libya

18:48 - February 05, 2011
Habari ID: 2075689
Kongamano la kimataifa la kuchunguza mpango wa kukabiliana na changamoto za kuuvunjia heshima Uislamu na Wislamu na kuzuia propaganda zinazochafua jila la dini hiyo litafanyika tarehe 6-8 Februari katika mji wa Zlitan nchini Libya.
Kongamano hilo litasimamiwa na Muungano wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu uliochini ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Kiislam ISESCO na Chuo Kikuu cha Sayansi za Kiislamu cha al Asmariyya.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kuchunguza mpango wa kuwaelimisha wanafunzi wa vyuo vikuu jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoukabili Uislamu na Waislamu.
Malengo mengine yametajwa kuwa ni kupanga mikakati ya pamoja ya kutekeleza mpango huo, kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi na jumuiya za Kiislamu katika nchi za Kiarabu, kusahihisha ripoti zisizokuwa sahihi kuhusu Uislamu na Waislamu huko Magharibi na kuonyesha sura sahihi ya ustaarabu wa Kiislamu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Koangamano hilo litahudhuriwa na wahadhiri wa vyuo vikuu, wasomi wa sekta ya mawasiliano, sayansi za Kiislamu, sheria za kimataifa na sayansi za jamii. 741883
captcha