IQNA

Katibu Mkuu wa OIC ataka kuadhimishwa Wiki ya Uratibu baina ya Dini'

13:59 - February 07, 2011
Habari ID: 2076748
Ekmeleddin Ihsanoglou Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amezitaka nchi zote za dunia kuadhimisha Wiki ya Kimataifa ya Uratibu baina ya Dini.
Ekmeleddin Ihsanoglou ametoa taarifa akiashiria hatua ya Umoja wa Mataifa ya kutenga tarehe 12 hadi 18 kuwa ni Wiki ya Kimataifa ya Uratibu baina ya Dini na kuitaka jamii nzima ya kimataifa kuadhimisha wiki hiyo.
Katibu Mkuu wa OIC amesema katika taarifa hiyo kwamba ni jambo la fahari kuona kwamba pendekezo la kutengwa wiki hiyo lilipendekezwa na Jordan, moja ya wanachama wa OIC na kupasishwa katika kikao cha 65 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Amesema OIC imeazimia kuheshimu na kunyanyua kiwango cha utamaduni wa uratibu na maelewano miongoni mwa wafuasi wa dini, staarabu na tamaduni tofauti duniani na kwamba tokea mwaka 1998 imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuimarisha utamaduni huo miongoni mwa nchi wanachama wa OIC.
Ihsanoglou amesisitiza kwamba jambo hilo lina umuhimu mkubwa hasa katika mazingira yanayotawala hivi sasa duniani. 742662
captcha