IQNA

Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa mazungumzo kati ya dini kufanyika India

17:23 - February 07, 2011
Habari ID: 2077061
Muungano wa Kimataifa wa Maulamaa wa Kiislamu umetangaza kuwa mkutano wa kwanza wa mazungumzo kati ya viongozi wa Kiislamu na wafuasi wa dini za Mashariki utafanyika New Delhi nchini India.
Mkutano huo wa siku tatu utaanza tarehe 19 Februari ukihudhuriwa na Makamu wa Rais wa India Hamid Ansari.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Malamaa wa Kiislamu Sheikh Yusuf Qaradhawi amesisitiza juu ya umuhim wa mkutano huo. Washiriki katika mkutano huo wanawakilisha jamii ya watu bilioni tatu.
Shekh Qaradhawi amesema kamati inayosimamia mkutano huo ilichukua uamuzi wa kuitisha mkutano wa wafuasi wa dini za Mashariki baada ya kukwama mazungumzo na Vatican kutokana na matamshi yaliyotolewa na Papa Benedict wa XVI dhidi ya Mtume Muhammad (saw). 743252
captcha