Kwa mujibu wa tovuti ya Islamic-events.be, kikao hicho kitafanyika katika Kituo cha Utamaduni, Uislamu na Masomo cha al-Hikma kuanzia saa nane alasiri. Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Geneva pia atashiriki katika kikao hicho.
Kikao cha Utamaduni na Kiislamu cha al-Hikma ni kituo kisicho cha kiserikali ambacho kinajishughulisha na masuala mbalimbali ya kidini, kiutamaduni, kijamii, kifamilia na kimasomo. Uandaaji wa mikutano, huduma za masomo ya kidini na kifamilia, intaneti, vipindi tofauti vya masomo, michezo na huduma za maktaba ni shughuli nyingine zonazofanywa na kituo hicho. 743792