Mashambulio hayo yaliyofanyika Jumatano alfajiri yamepelekea wakazi wa ukanda huo wakiwemo watoto na wanawake kujeruhiwa vibaya wangine wakiwa hali mahututi.
Akibainisha suala hilo, Ad'ham Abu Salmaya Msemaji wa Kamati ya Misaada ya Dharura ya Gaza amesema kuwa katika moja ya mashambulio hayo, ndege za kivita za utawala huo ghasibu zilishambulia moja ya maghala ya kuhifadhia madawa na vifaa vya tiba na kuharibu kila kitu kilichokuwemo humo.
Jeshi la utawala huo ghasibu limedai kuwa limefanya mashambulio hayo katika kujibu mashambulio ya maroketi ya Wapalestina na pia kuharibu mahandaki yanayotumiwa na eti magaidi wa Kipalestina.
Ni kwa muda wa miaka minne sasa tokea Wazayuni waanze kutekeleza mzingiro wa kidhulma dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi, mzingiro ambao unaandamana na mashambulio ya mara kwa mara ya Wazayuni dhidi yao. 745294