IQNA

Kongamano la Kimataifa la Kumtetea Mtume laanza Mauritania

17:27 - February 13, 2011
Habari ID: 2080308
Kongamano la kimataifa la kielimu la kumtetea Mtume Muhammad (saw) lilianza jana katika mji mku wa Mauritania, Nouakchott.
Shirika rasmi la habari la Mauritania limeripoti kuwa kongamano hilo linafanyika chini ya anwani ya “Taathira za ustaarabu kwa Waislamu kati ya uongofu wa Uislamu na changamoto za dunia ya sasa”.
Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Mauritania Muhammad al Mukhtar amehutubia kongamano hilo akisisitiza juu ya udharura wa kushikamana na Uislamu halisi na kusema hakika ya dini ya Kiislamu ni kutumia vyema elimu katika kila zama na mahala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Utamaduni ya Kiislamu ya Mauritania Muhammad al Hafidh al Nahwi pia amehutubia kongamano hilo linalohudhuriwa na wasomi wa nchi za Kiarabu na kigeni akisisitiza juu ya umuhimu wake. Amemshukuru Rais wa Mauritania kwa huduma zake kwa dini ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na kuasisi Redio Qur’ani Tukufu na kiwanda cha kuchapisha Qur’ani. Amesisitiza juu ya umuhimu wa kuiga maadili bora ya Mtume Muhammad (saw) na kusema kuwa suala hilo linamtayarisha mwanadamu kufikia daraja za juu za ukamilifu. 747013
captcha