Jumuiya ya Kimataifa ya Uarifishaji Uislamu na Uungaji Mkono kwa Mtume Mtukufu (saw) itaandaa hivi karibuni maonyesho ya kuarifisha tabia na maadili bora ya Mtume Mtukufu (saw) huko London, mji mkuu wa Uingereza.
Jumuiya hiyo inayofungamana na Taasisi ya Kimataifa ya Uislamu imeandaa maonyesho saba kama hayo ya kumuarifisha duniani Mtume Muhammad Mustafa (saw) katika miji mbalimbali na ya hivi karibuni zaidi yalifanyika Vienna, mji mkuu wa Austria.
Jumuiya hiyo pia imeandaa masomo 30 maalumu ya kumuarifisha Mtume Mtukufu katika nchi za Magharibi ambapo wanafunzi 2,700 wameshiriki.
Jumuiya hiyo hadi sasa imeanzisha tovuti sita tofauti kwa lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kichina na Kituruki kwa lengo la kumuarifisha Mtume Mtukufu (saw). 747617