Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo la siku moja limefanyika leo Februari 14 katika Taasisi ya Kisiasa na Utafiti wa Kimataifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran mjini Tehran.
Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa. Kongamano hilo ni la kwanza katika mfululizo wa vikao vyenye anuani ya: "Udiplomasia, Qur'ani na Changamoto za Dunia ya Leo".
Kati ya waliozungumza katika kikao hicho ni Hujjatul Islam Mohsen Qaravian ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa cha Qum na vilevile Dkt. Hussein Shafie, mwanachama wa bodi ya Chuo Kikuu cha Tarbiat Mualim cha Tehran.
746966