IQNA

Wazayuni wamvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw)

15:44 - February 16, 2011
Habari ID: 2081939
Wazayuni wanaoishi katika kijiji kimoja huko magharibi mwa Ramallah katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu wamechukua hatua ya dharau dhidi ya Mtume Mtukufu (saw) kwa kuandika maandishi ya kumkosea heshima mtukufu huyo katika kuta za nyumba zao.
Wameandika maandishi hayo kwa Kiarabu na kuchora mchoro wa nyota ya utawala wa Kizayuni pembeni yake.
Ni vyema kukumbusha hapa kwamba vitendo kama hivyo vya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu vimekuwa vikifanywa mara kwa mara na Wazayun katika mji wa Ramallah.
Hivi karibuni walowezi kadhaa wa Kizayuni waliihujumu haram ya Hadhrat Yusuf (as) katika mji wa Nablos kaskazini mwa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan huku wakisaidiwa na kupewa himaya na askari wa utawala ghasibu wa Israel. 748436
captcha