IQNA

Kongamano la Umoja wa Kiislamu laanza Tehran

11:42 - February 19, 2011
Habari ID: 2082818
Karibu wasomi 250 mashuhuri wa Kiislamu kutoka nchi 57 wanahudhuria Kongamano la 24 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mjini Tehran kuanzia Februari 19-21 ambapo suala la matukio ya hivi karibuni katika ulimwengu wa Kiislamu linapewa umuhimu.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri amesema kuwa kongamano hilo la Umoja wa Kiislamu litaangazia pia mikakati ya kuimarisha ukuruba wa madhehebu ya Kiislamu.
Ayatullah Taskhiri ameashiria matukio ya kihistoria katika nchi kadhaa za Kiarabu na kusema kuwa kongamano lijalo la umoja wa Kiislamu litaangazia kwa kiwango kikubwa matukio hayo.
Aidha amesema kongamano la mwaka huu litatathmini makongamano 20 yaliyopita ya Umoja wa Kiislamu.
Kati ya wanaohudhuria kongamano hilo ni Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Dkt. Sayyid Muhammad Husseini Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu.
Pembizoni mwa kongamano hilo kutakuwa na maonyesho ya vitabu kuhusu kukurubisha madhehebu ya Kiislamu.
749743
captcha