IQNA

Kiongozi wa Mashia wa Bahrain alaani vikali mauaji ya wananchi

15:57 - February 19, 2011
Habari ID: 2083253
Ayatullah Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa Mashia wa Bahrain katika hotuba aliyotoa kwenye swala ya Ijumaa ya jana tarehe 18 Februari katika Msikiti wa Imam Swadiq (as) mjini Ad-Duraz, amelaani vikali mauji ya wananchi katika medani ya Lulu mjini Bahrain.
Amesema kitendo hicho kilichotekelezwa na jeshi la Bahrain ni mauaji ya umati na ya makusudi moja kwa moja ambayo hayawezi kuhalalishwa kwa kisingizio chochote kile eti cha kutawanya maandamano.
Ayatullah Qassim amesema usalama wa wananchi wa Bahrain unahatarishwa na serikali ya Manama yenyewe. Ayatullah Sheikh Isa Qassim ameitaka jamii ya kimataifa kuwajimbika mbele ya mauaji na matukio yanayoendelea hivi sasa nchini Bahrain.
Amewataka wananchi wa Bahrain pia kuimaraisha umoja wao na kutokubali kutenganishwa. Amesema mauaji na ukandamizaji unaofanywa na jeshi la Bahrain dhidi ya waandamanaji unaondoa kabisa uwezekano wa kufanyika mazungumzo kati ya pande mbili. 750045
captcha