IQNA

Mashindano ya Qur'ani kufanyika Virginia, Marekani

17:05 - February 19, 2011
Habari ID: 2083424
Mashindano ya sita ya kuhifadhi Qur'ani tukufu yamepangwa kufanyika tarehe 27 Februari katika Kituo cha Kiislamu cha Virginia (CVQC) katika mji wa Richmond huko Marekani.
Mashindano hayo yatafanyika kwa lengo la kuwahamasisha Waislamu kusoma Qur'ani Tukufu na kueneza mafundisho yake katika makundi ya watoto na watu wazima.
Katika sehemu ya watu wazima washiriki watachuana katika kuhifadhi sura kadhaa za juzuu amma, juzuu nzima na juzuu tano. Na sehemu ya washiriki watoto watachuana kuhifadhi sura kadhaa za Qur'ani Tukufu.
Majaji wa mashindano hayo watachunguza uwezo wa washindani na jinsi wanavyolinda sheria za tajwidi.
Majina ya washidi yatatangazwa tarehe 6 Machi na kutunukiwa zawadi. 750268

captcha