Ja'far Abdu Salaam, Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu amesema kuwa mapinduzi ya Misri yaliyopelekea kuangushwa kwa serikali ya Rais Hosni Mubarak wa nchi hiyo ni mwanzo wa mwamko katika nchi za Kiislamu.
Akizungunza hapo katika kikao cha 24 cha Wiki ya Umoja wa Kiislamu Ja'far Abdu Salaam, amesifu matamshi ya Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na matukio ya hivi karibuni ya Misri na kutoa shukrani zake za dhati kwa uungaji mkono wa taifa la Iran kwa watu wa Misri katika mapambano yao ya kumng'oa madarakani dikteta Hosni Mubarak. Akibainisha sababu zilizopelekea Mubarak ang'olewe madarakani, Abdu Salaam amesema kuwa hali mbaya ya kiuchumi na dhulma iliyofanywa na serikali yake katika ugawaji wa utajiri wa nchi hiyo kwa matabaka tofauti ya wananchi ni baadhi ya mambo yaliyowachukiza mno wananchi hao na kuwapelekea wamfukuze madarakani kiongozi huyo kibaraka wa nchi za Magharibi.
Amesema jambo jingine ambalo bila shaka litapelekea mataifa ya Kiarabu kusimama dhidi ya watawala dhalimu ni kutokuwepo demokrasia wala kuheshimiwa haki za binadamu katika nchi hizo. Amesema hii ni mbali na ukweli kuwa mataifa hayo yanataka kutekelezwa mafundisho ya Kiislamu katika nchi zao. 750503