Kongamano hilo lililofanyika Februari 19 limehudhuriwa na shakhsia wa kimataifa.
Kati ya waliohudhuria ni Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (bunge) na Abdullah Safiyuddin Mkuu wa Idara ya Hizbullah mjini Tehran.
Katika hotuba yake Larijani amesema harakati ya Imam Khomeini MA ilitufunza namna ya kukabiliana na fitina za kimadhehebu. Amesema harakati hiyo ya Imam Khomeini ina mizizi katika harakati ya mwanzoni mwa Uislamu.
Kuhusu shakhsia ya kishujaa ya Imad Mughniya, Larijani amesema ,'alikuwa na nafasi kubwa katika kuwatimua wanajeshi vamizi wa Kizayuni kusini mwa Lebanon'. Larijani amesema harakati za mwamko wa wananchi huko Misri, Tunisia, Yemen na Bahrain zimepata ilhamu kutoka Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na maelfu ya mashahidi kama vile Imad Mughniya.
Ameongeza kuwa mashujaa shahidi katika ulimwengu wa Kiislamu walijitahidi sana kuleta mwamko wa Kiislamu katika jamii.
Larijani ametoa salamu zake za pongeze kwa umma wa Kiislamu kwa mnasaba wa kumbukumbu kuzaliwa Mtume Muhammad SAW na Imam Sadiq AS.
750669