IQNA

Mashindano ya Qur'ani na hadithi za Mtume kwa vijana wa Qatar

16:20 - February 22, 2011
Habari ID: 2084848
Kitengo cha shughuli za vijana cha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi ya Qatar kinajitayarisha kuandaa duru ya 24 ya mashindano ya Qur'ani Tukufu na hadithi za Mtume kwa vijana wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Qatar la as-Sharq, mashindano hayo yatakayofanyika katika Klabu ya Michezo ya al-Arabi ya mjini Doha, kati ya tarehe 27 Februari hadi 8 Machi yatawashirikisha washindani 65 kutoka taasisi na vituo 16 vya vijana wa Qatar.
Akizungumzia suala hilo Jamal Faizi mkuu wa kitengo kilichotajwa amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika fremu ya shughuli za kuchaguliwa Doha kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka uliopita wa 2010. 751686
captcha