IQNA

OIC yataka mbinu za amani zitumike katika nchi zenye migororo

14:28 - February 23, 2011
Habari ID: 2085373
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC imetoa wito kwa nchi zote za Kiislamu zinazokumbwa na migogoro kutumia mbinu za amani kwa ajili ya kutuliza hali ya mambo na kujiepusha na machafuko na umwagaji damu.
Katibu Mkuu wa OIC Prof. Ekmeleddin Ihsanoglu ametoa taarifa akisema jumuiya hiyo ina wasi wasi kuhusu matukio yanayojiri katika nchi za Kiislamu.
OIC imesikitishwa na watu kupoteza maisha na mali kuharibiwa katika ghasia zinazozikumba baadhi ya nchi za Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati.
“Ni wazi kuwa nchi hizo zinapita katika kipindi kigumu na kunahitajika subira, hekima na busara ya kutazama mustakbali katika kukabliana na yanayojiri”, amesema Ihsangolu.
Amesisitiza kuwa OIC ina uhakika kuwa wananchi katika nchi husika watavuka kipindi hiki kigumu kwa maelewano na amani.
Amesema matakwa ya Waislamu duniani ya kutaka utawala bora, utawala wa sheria, kuheshimiwa haki za binadamu, kupambana na ufisadi, kupanuliwa harakati za kisiasa na maendeleo ni mambo ambayo yanatambuliwa katika Hati ya OIC kama misingi muhimu.
“OIC ina uhakika kuwa mataifa makubwa ya umma wa Waisalmu yana uwezo, pasina uingiliaji wa kigeni, kukabiliana na changamoto zilizopo katika kuelekea kwenye mustakabali wa ustawi na maendeleo’.
752442

captcha