Hayo ni kwa mujibu wa Mahdi Nadi, Mkuu wa Taasisi ya Darul Qur'an inayofungamana na Shirika la Maendeleo ya Kiislamu la Iran.
Bajeti hiyo inalenga kuhimiza umma katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki katika harakati za Qur'ani na kuunga mkono vituo vya Qur'ani.
Kwa wastani kila taasisi ya Qur'ani ya Tehran itapokea Riali milioni tano katika kipindi cha Februari 20 hadi Machi 30.
Amesema kuna mipango ya kuongeza misaada kwa ajili ya vituo vya Qur'ani katika vijiji vya mkoa wa Tehran. Amesema kuna vituo 45 vya mafunzo ya Qur'ani katika vijiji vya mkoa wa Tehran.
752117