Hujjatul Islam Mohsen Qara'ati amesema kila wakati mwanadmau anapotafakari kwa kina kuhusu aya za Qur'ani anapata hekima na busara mpya kutoka katika kitabu hicho kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.
Sheikh Qara'ati ambaye pia ni Mkuu wa Kamati ya Kutathmini Zakat amesema uenezwaji mafundisho ya Qur'ani ni jambo linalopaswa kupewa uzito mkubwa.
Akizungumza katika kongamano la kuwaenzi wanaofanya harakati katika uga wa Zaka nchini Iran, amesema Qur'ani inaitaja Zaka na Khums kuwa sadaka na kusema hilo linaonyesha ikhlasi na imani. Ameongeza kuwa Uislamu unasimama kwa nguzo tano ambapo Zaka ni mojawapo ya nguzo hizo lakini la kusikitisha ni kuwa Zaka haitiliwi maanani sana.
Kongamano la kuwaenzi wanaharakati katika uga wa Zaka na masuala ya kutoa misaada lilifanyika Februari 23 katika mji mtakatifu wa Qum.
752650