Ameongeza kwamba ari ya wananchi ya kuwafukuza watawala madikteta inakwenda sambamba na mafunzo ya Kiislamu yanayosisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo viongozi waadilifu.
Ayatullah Kashani amesema ulimwengu wa Kiislamu umegundua kuwa unakabiliwa na uadui mkubwa kutoka nchi za Magharibi na kwa mantiki hiyo umeamua kufuata nyayo za Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (MA) aliyejitokeza na kupinga wazi wazi utawala wa kiimla wa mfalme Shah Pahlavi mwaka 1979 na hatimaye akafanikiwa kumpindua mfalme huyo kwa msaada wa wananchi wa Iran.
Hatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran aidha ametoa mwito wa kudumishwa na kuimarishwa zaidi umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.
753366