IQNA

Hijabu yapata umashuhuri tena Tunisia

9:27 - February 26, 2011
Habari ID: 2086091
Wanawake Waislamu nchini Tunisia wameanza kupata matunda ya mapinduzi nchini humo kwani sasa wana uhuru wa kuvaa vazi la stara la Kiislamu, Hijabu, hadharani.
Baada ya miaka mingi ya kukandamizwa na utawala wa dikteta Ben Ali aliyetimuliwa mwezi jana, sasa wanawake wanaovaa hijabu wanaweza kuonekana mitaani na katika taasisi za umma.
Waziri wa Masuala ya Kidini wa Tunisia Laroussi Mizouri ametangaza kuwa hijabu ni suala la mtu binafsi na sehemu ya haki za mwanamke.
Wakati wa utawala wa rais wa kwanza wa Tunisia Habib Bourguiba, vazi la hijabu ilipigwa marufuku hadharani sera ambayo iliendelezwa na mrithi wake Zine el Abidine Ben Ali ambaye ametimuliwa madarakani hivi karibuni.
Tokea siku ya ushindi wa mapinduzi ya Tunisia, Januari 14, miji ya Tunisia imeshuhudia ongezeko kubwa la wanawake wanaojisitiri kwa vazi la hijabu.
Itakumbukwa kuwa utawala wa Ben Ali pia ulikuwa umepiga marufuku adhana, sala za jamaa na sala ya Ijumaa nchini Algeria.
753364
captcha