IQNA

Mahfali ya kufarijika na Qur'ani mjini Seihat Saudi Arabia

15:23 - February 26, 2011
Habari ID: 2086408
Duru ya sita ya mahfali ya kimataifa ya usomaji Qur'ani Tukufu ambayo imewajumuisha wasomaji mashuhuri wa Qura'ni kutoka nchi za Ghuba ya Uajemi imefanyika huko katika mji wa wakazi wengi wa Kishia wa Seihat nchini Saudi Arabia.
Mahfali hiyo iliyoandaliwa na Kamati ya An'war al-Qur'an ya mji huo ilifanyika siku ya Alkhamisi kwa mnasaba wa kuzaliwa Mtume Muhammad (saw) pamoja na mjukuu wake Imam Jaffar as-Swadiq (as).
Mbali na wasomaji mashuhuri wa Qur'ani kutoka nchi za Ghuba ya Uajemi, shakhsia na wanazuoni wa kidini na kijamii pamoja na wakuu wa taasisi na jumuiya za Qur'ani kutoka nchi hizo walishiriki katika mahfali hiyo iliyofanyika katika Msikiti wa Rasul al-A'dham (saw).
Akizungumza katika mahfali hiyo, Habib Yusuf, mwanachama wa kamati iliyotajwa alisema kuwa mahfali hiyo ni moja ya shughuli za kila mwaka ambazo huandaliwa na kamati hiyo kwa lengo la kuwapa wasomaji Qur'ani wa kieneo fursa ya kubadilishana uzoefu, kuarifishwa ratiba za elimu, masomo na mbinu za ufundishaji pamoja na kusikiliza sauti nzuri na za kuvutia za wasomaji Qur'ani hao wa kieneo.
Kamati ya Anwar al-Qur'an ni taasisi inayojishughulisha na masuala ya masomo ya Qur'ani Tukufu na tajwidi. 753566
captcha