Vikao vya pamoja vya wataalamu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kuhusu elimu na uandishi magazeti vimepangwa kufanyika kesho tarehe 27 Februari hadi Machi Mosi huko Rabat mji mkuu wa Morocco.
Kwa mujibu wa tovuti ya ISESCO, vikao hivyo vimepangwa kujadili njia za kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili katika Taasisi Kuu ya Elimu na Mawasiliano ISIC katika mji huo. Washiriki wa vikao hivyo wanatazamiwa kujadili mabadiliko ya mbinu za mafunzo ya uandishi magazeti katika taasisi zinazotoa masomo hayo.
Wakuu wa taasisi hizo na pia walimu wanaotoa masomo hayo na wamiliki wa mashirika ya vyombo vya habari vya Morocco, Algeria, Tunisia na Ufaransa na vilevile wawakilishi wa Mfuko wa Ustawi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wanawake INIFEM na Wakala wa Ushirkiano wa Kiufundi wa Morocco na Ujerumani GTZ wamealikwa kushiriki katika vikao. 753577