As-Suweidan amesema kuwa watawala wanapasa kuwa waadilifu na kufanya usawa kati ya raia wao wa Kishia na Kisuni kwa sababu utawala unaodumu ni ule uliochaguliwa na wananchi na unaoheshimu maoni yao.
Sheikh As-Suweidan amesema anashangazwa kuona kuwa mapambano ya wananchi wa Bahrain yanapingwa na kupuuzwa na baadhi ya mirengo na makundi kinyume na mapambano yanayofanyika katika nchi nyingine za Kiarabu dhidi ya tawala dhalimu na za kidikteta, katika hali ambayo Mashia pia wana haki na utukufu kama wananchi wa nchi zingine za Kiarabu.
As-Suweidan amesema kuwa inashangaza kuona kwamba Bahrain ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu wa madhehebu ya Shia inatawaliwa na Wasuni ambao wanawabagua na kuwanyima haki zao, dhulma ya muda mrefu ambayo amesema inatokana na matukio ya kihistoria.
Mhubiri na mwanaharakati huyo wa Kuwait amesema kuwa anashangazwa mno na watu ambao wanaunga mkono maandamano na harakati za kupigania haki, demokrasia na uhuru katika nchi za Misri, Tunisia na Libya lakini wanapinga harakati kama hizo za marekebisho ya kisiasa nchini Bahrain. Amesema msimamo wa kindumakuwili wa Marekani kuhusiana na suala la haki za mataifa kujiainishia mustakabali na uhuru wao ni wa kuaibisha sana. 754616