Kwa mujibu wa tovuti ya Moheet, kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kiarabu ya Falaki na Sayansi za Anga za Juu (AUASS) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Sayansi za Kiislamu huko Amman, Jordan.
Makundi ya kisayansi kutoka nchi za Kiislamu na Kiarabu yatashiriki katika kongamano hilo ambapo makala 50 za utafiti zitawasilishwa.
Kongamano hilo linalenga kuchunguza mafanikio muhimu kuhusu mbinu za kuainisha nyakati maalumu za kufanyika ibada kwa mujibu wa mwezi mwandamo katika sayari ya dunia.
Awni Al-Khasawneh mkurugenzi mkuu wa jumuiya hiyo amesema utafiti uliofanywa na wanazuoni Waislamu na wanafalaki wa Jordan ni kati ya mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo. Amesema washiriki watawasilisha mapendekezo yao kuhusu njia za kuonekana mwezi mwandamo katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Jumuiya ya Kiarabu ya Falaki na Sayansi za Anga za Juu yenye makao yake mjini Amman ilizinduliwa mwaka 1998 kwa lengo la kustawisha sayansi za falaki na kufafanua nafasi ya utafiti wa Kiislamu katika uga huo.
755251