Kituo cha habari cha 234next kimeripoti kuwa mkaguzi wa jela ya jimbo la Zamfara Abu Bakr Falke amesema katika sherehe ya kuhitimisha masomo hayo kuwa yametolewa kwa wafungwa kwa lengo la kueneza misingi ya maadili ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa mbali na masomo ya Qur'ani wafungwa hao pia wamepata masomo mengine yatakayowawezesha kuendesha maisha yao baada ya kutumikia vifungo bila ya kutegemea watu wengine.
Abu Bakar Falke amesema wafungwa waliopata mafunzo hayo na elimu ya ufundi watasamehewa na amewataka watilie maana misingi ya madili mema.
Gavana wa jimbo la Zamfara Mahmud Shinkafi pia amehutubia sherehe hiyo akiwashukuru maafisa wa jela hiyo. Amesema kuanzisha masomo ya kiraa ya Qur'ani kwa wafungwa kutapelekea kupungua matatizo na uhalifu katika jamii.
Mke wa gavaza huyo Aisha Shinkafi pia amewazawadia nakala ya Qur'ani wafungwa wote wa jela ya Zamfara na washindi 50 kati yao wamepewa tuzo nyinginezo. 755150