IQNA

Kenya kuruhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu

20:16 - March 02, 2011
Habari ID: 2089475
Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itapitisha sheria ya kuondoa vivingiti vya kodi katika kuchapishwa Hati ya Dhamana ya Kiislamu kabla ya kumalizika mwaka 2011.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kenya inatazamia kuzindua Hati za Dhamana za Kiislamu maarufu kama Sukuk ifikapo mwishoni mwa mwaka.
Kenya ambayo ina uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki bado haijaweza kupenya katika soko la kimataifa la hati za dhamana za kawaida na kwa hivyo inajaribu kutumia hati za dhamana za Kiislamu kupata fedha kutoka wawekezaji wanaozingatia sheria za Kiislamu, amesema Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Profesa Njuguna Ndung'u kupitia barua pepe.
"Tumepokea maombi ya mradi ambao tutautaja na unaweza kugharamiwa kupitia fedha zitakazopatikana kwa kuchapisha hati za sukuk", amesema Ndung'u.
Benki Kuu ya Kenya iliwahi kupata fedha za miradi ya miundo mbinu kupitia fedha za sukuk mwaka 2009. Hata hivyo ukosefu wa sheria za kodi ni kizingiti kikubwa katika ustawi wa soko la sukuk nchini Kenya.
Bara la Afrika limekuwa eneo la ustawi mkubwa wa mfumo wa kifedha wa Kiislamu huku nchi kama vile Senegal na Afrika Kusini zikijitahidi kuanzisha mfumo wa benki za Kiislamu na hati za dhamana za Kiislamu, sukuk.
Kenya sasa inataka kuwa kituo kikuu cha mfumo wa kifedha wa Kiislamu barani Afrika na inapanga kutoa huduma zaidi za kifedha za Kiislamu.
Weledi wanasema huku eneo la kaskazini mwa Afrika lilikumbwa na misukosuko ya kisiasa, Kenya inatazamia kutumia fursa hiyo kuwavutia wawekezaji kutoka nchi zenye utajiri wa mafuta za Ghuba ya Uajemi.
Kenya ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika Mashariki na Kati kuanzisha benki za Kiislamu mwaka 2007.
756151

captcha