IQNA

Nuskha za hati za Kiislamu nchini Mali zinakaribia kutoweka

20:07 - March 02, 2011
Habari ID: 2089476
Mkuu wa masuala ya kiutamaduni katika mji wa Timbuktu nchini Mali amezungumzia nafasi muhimu na nuskha za hati za Kiislamu katika kuhifadhi turathi za Waislamu wa nchi hiyo na kuelezea wasi wasi wake kuhusu uwezekano wa kutoweka hati hiyo kutokana na kupuuzwa na taasisi husika.
Kwa mujibu mwa mwandishi wa IQNA magharibi mwa Afrika, Sayyid Ali Ould Sidi ambaye ni mkuu wa masuala ya utamaduni wa Timbuktu amesema: "Nyaraka na nuskha za hati za Kiislamu zilizoko Timbuktu lazima zitambuliwe na kurekebishwa kwa sababu hili lisipofanyika, turathi za mji huo ambazo zimepuuzwa zitatoweka".
Naye Waziri wa Utamaduni wa Mali Sheikh Omar Sissoko amezungumzia suala hili na kusema: "Iwapo Mali haitaweza kuhifadhi nuskha hizi za Kiislamu ili kuziokoa, hatutakuwa na budi ila kuziomba taasisi za kimataifa kutusaidia katika kazi hii muhimu haraka iwezekanavyo".
Athari za kipekee za Kiislamu za Mali zinazojumuisha vitabu vya kale katika mji wa Timbuktu zina umri wa zaidi ya karne tano na zinahesabiwa kuwa fahari ya Uislamu barani Afrika.
756663
captcha