Taarifa hiyo imetolewa na Hamas kufuatia kuongezaka vitendo vya uharibifu vinavyotekelezwa mara kwa mara na utawala ghasibu wa Israel katika eneo la kusini mwa Msikiti wa al-Aqsa kwa shabaha ya kujenga huko hekalu bandia la Mayahudi. Katika taarifa hiyo yenye maneno makali Hamas imelaani vikali uchochezi na uharibifu huo wa Wazayuni wanaotumia vibaya hali iliyojitokeza katika Mashariki ya Kati kwa madhumuni ya kuzidisha kasi ya uharibifu wa maeneo ya kihistoria ya Kiislamu na Kiarabu katika mji huo. Taarifa hiyo imesema kuwa uharibifu huo ni dharau ya wazi ya utawala huo kwa taifa la Palestina na umma wa Kiislamu na Kiarabu. Imesema licha ya uharibifu unaofanywa na Wazayuni katika eneo hilo lakini jambo hilo halitaathiri chochote katika kutambuliwa rasmi eneo hilo kuwa ni la Kiarabu na Kiislamu na kwamba taifa la Palestina litaendelea kupigania kwa nguvu zake zote haki zake zinazokanyagwa na utawala ghasibu wa Israel. Imeendelea kusema kuwa taifa la Palestina llitaendelea kujivunia Quds kama nembo ya umma wa Kiislamu na Kiarabu. Mwishoni mwa taarifa hiyo Hamas imeitaka Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na taasisi za kimataifa za haki za binadamu kuchukua hatua za haraka ili kutetea athari za kihistoria na Kiislamu katika eneo la Msikiti wa al-Aqsa. 758888