IQNA

Duru ya saba ya mashindano ya Qur'ani kuanza mjini Kansas City Marekani

15:03 - March 07, 2011
Habari ID: 2091524
Duru ya 7 ya mashindano ya Qur'ani Tukufu inatazamiwa kuanza hivi karibuni katika mji wa Kansas City nchini Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao wa ickansas washiriki wa mashindano hayo watachuana katika vitengo vinne vya kuhifadhi sura za A'ala hadi Nas, sura ya Jinn, Dhariyaat na sura ya Mu'minuun. Washiriki wa mashindano hayo wanaweza kushiriki katika zaidi ya kitengo kimoja, isipokuwa katika hatua ya kwanza ambayo inawahusu watoto walio na umri wa chini ya miaka 10 tu. Hatua ya utangulizi ya mashindano hayo itafanyika tarehe 20 Machi na tarehe ya kufanyika hatua ya mwisho kutangazwa na waandaaji hapo baadaye ambapo washindi watatunukiwa zawadi katika sherehe maalumu. 758867
captcha