IQNA

Tarjumi mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kihispania

15:42 - March 07, 2011
Habari ID: 2091924
Tarjumi mpya kabisa ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kihispania itazinduliwa Machi 8 katika Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tarjumi hiyo itazinduliwa na Bw. Mohammad Baqer Khorramshad Mkuu wa ICRO na Hujjatul Islam Rabbani Mkurugenzi wa Taasisi ya Andishe-ye-Sharq, mtarjumi, wataalamu wa utamaduni na wataalamu na wanafunzi wa lugha ya Kihispania.
Tarjumi hiyo imechapishwa na Kituo cha Tartjumi na Uenezi wa Mafundisho ya Kiislamu kwa ushirikiano na Taasisi ya Andishe-ye-Sharq.
Baada ya kuzinduliwa tarjumi hiyo kutakuwa na kikao cha kutathmini tarjumi ya "Kitabu cha Nne cha Mathnawi" na “Bar Karane-ye Chehel Hadith” kilichoandikwa na Imam Khomeini MA. Kikao hicho pia kitachunguza Tarjumi ya Kiingereza ya "Dastan-e-Rastan" na "Imam Ali AS na Amani ya Dunia" .
759448
captcha