Imetambulika kuwa mfumo wa kifedha wa Kiislamu ndio njia bora zaidi kwa Russia na Nchi za Jumuiya ya Madola Huru CIS (Nchi zilizokuwa Shirikisho la Sovieti kabla ya kupata uhuru).
Katika mkutano kuhusu 'Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu Russia na CIS' uliofanyika wiki iliyopita mjini Istanbul, masuala kuhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu yalijadiliwa.
Kati ya nchi za CIS ni Tajikistan na Kazakhstan zilizotangaza kuwa tayari kuanzisha mfumo wa kifedha wa Kiislamu.
Kikao hicho kimeonelea kuwa kuna haja ya kuwaelimisha maafisa wa kifedha wa Russia na CIS kuhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu.
759401