IQNA

Mahfali ya kufarijika na Qur'ani yafanyika Gaza

14:15 - March 08, 2011
Habari ID: 2092225
Duru ya kumi ya mahfali ya kufarijika na Qur'ani Tukufu ilifanyika siku ya Jumapili tarahe 6 huko katika Ukanda wa Gaza.
Mahfali hiyo iliyoandaliwa na kitengo cha hifdhi ya Qur'ani ya Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Ghaza kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Misikiti ya ad-Durj ilifanyika katika Msikiti wa al-Aibki.
Viongozi mbalimbali wa masuala ya utamaduni na masuala ya kidini walihudhuria mahfali hiyo iliyofana sana. Wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Ukanda wa Gaza walishiriki katika mahfali hiyo na kuwafariji washiriki kwa sauti zao nzuri za usomaji Qur'ani.
Mashindano ya Qur'ani pia yalifanyika pembezoni mwa mahfali hiyo ya kuvutia.
Akizungumza katika mahfali hiyo Mundhar al-Gumari, Mkurugenzi wa Idara Kuuya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Gaza alisema kuwa kuna udharura mkubwa wa kuimarisha usomaji wa Qur'ani kwa sauti na mbinu tofauti katika jamii ya Palestina na kuongeza kuwa idara yake iko tayari kushirikiana na upande wowote ule utakaochukua jukumu la kufuatilia jambo hilo. 759360
captcha