IQNA

Qur'ani kutarjumiwa kwa lugha ya ishara nchini Marekani

13:04 - March 10, 2011
Habari ID: 2093508
Qur'ani Tukufu itatarjumiwa hivi karibuni kwa lugha ya ishara nchini Marekani ili kuwawezesha viziwi kunufaika na mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Starttribune mpango wa kutekelezwa tarjumi hiyo utatekelezwa na tawi la Taasisi ya Kimataifa ya Waislamu Viziwi la Minnesota Marekani.
Marley Shirley mwanachama wa baraza la uongozi la taasisi hiyo amesema kwamba kuna uhaba mkubwa wa vitabu vya Kiislamu kwa ajili ya watu wasiosikia nchini Marekani.
Amesema kuna mipango ya kufanyika mkutano wa kukusanya pesa kwa ajili ya kudhamini bajeti ya kutarjumiwa Qur'ani Tukufu kwa lugha ya ishara kwa ajili ya viziwi wa Minnesota.
Taasisi iliyotajwa ya viziwi kabla ya hapo imekuwa ikitoa msaada wa kuwawezesha viziwi kunufaika na hotuba za swala Ijumaa zinazotolewa katika jimbo hilo la Minnesota. 760925
captcha