IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanajeshi yaanza Saudi Arabia

16:29 - March 12, 2011
Habari ID: 2093795
Duru ya sita ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanajeshi yameanza leo Ijumma huko katika mji mtakatifu wa Mkaka nchini Saudi Arabia. Mashindano hayo yatasimamiwa na Sultan bin Abdul Aziz, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo.
Abdallah bin Swaleh bin Abdul Hamid Aal Sheikh Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Masuala ya Kidini katika Jeshi la Saudia amesema kuwa mashindano hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwashwawishi wanajeshi wa nchi mbalimbali za Kiislamu wahifadhi kitabu hicho kitakatifu na kueneza mafundisho yake jeshini. Amesema mahafidh 90 kutoka nchi 20 za Kiislamu wanashiriki katika mashindano hayo. Duru ya kwanza ya mashindano hayo ilifanyika nchini Saudia mwaka 2001. 761542
captcha