Mashindano hayo yanasimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Kiislamu ISESCO.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kutoa huduma kwa watoto wadogo ambao hawawezi kupata huduma za ISESCO nchini Chad.
Malengo mengine yametajwa kuwa ni kuhamasisha watoto kuhifadhi Qur'ani na kunyanyua juu nafasi ya shule za Qur'ani hususan katika maeneo ya kaskazini mwa Chad.
Washindi katika mashindano hayo watatunukiwa zawadi katika sherehe itakayohudhuriwa na mwakilishi wa ISESCO katika Wizara ya Elimu ya Chad Bwana Ali Muhammad Swaleh. 764719