IQNA

Uandikishaji wa majina ya duru ya tano ya mashindano ya Qur'ani waanza Imarati

19:56 - March 16, 2011
Habari ID: 2097142
Kamati inayoandaa duru ya tano ya mashindano ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la 'usomaji bora wa Qur'ani Tukufu' katika mwaka huu wa 2011 imeanza kuandikisha majina ya watu walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Bayan linalochapishwa nchini Imarati, Ibrahim Muhammad Bumulihha, mkuu wa kamati hiyo amesema kuwa mashindano hayo yatakayofanyika katika hatua tano yatawajumuisha vijana walio chini ya umri wa miaka 15, vijana wa miaka 15 hadi 25, vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 26, kundi la maimamu wa misikiti na waadhini.
Amesema watu wate walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo ya usomaji Qur'ani au adhana wanaweza kufanya hivyo bila kizuizi chochote.
Muhammad Swafar as-Suweidi mmoja wa wasimamizi wa mashindano hayo amesema hatua ya awali ya mashindano hayo itafanyika ambapo wasomaji bora 10 katika kila kundi watachaguliwa kwa ajili ya kushiriki katika hatua ya baadaye.
Washiriki watapaswa kujaza fomu za usajili zinazotolewa na kamati hiyo au kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tuzo ya Dubai au kupitia intaneti. 764889
captcha