Akizungumza na balozi wa Uturuki mjini Tehran, Dakta Ali Larijani ameongeza kuwa, vikosi vya kigeni vinatenda jinai kubwa kwa kuwakandamiza wananchi wa Bahrain ambao wanapigania haki zao kwa misingi ya demokrasia. Wakati huohuo, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran imemuita nyumbani balozi wake aliyeko mjini Manama. Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni kulalamikia mauaji ya kinyama yanayofanywa na majeshi ya Bahrain na yale ya nchi za Kiarabu nchini humo. Balozi Mehdi Agha- Jafari aliteuliwa kuwa balozi wa Iran nchini Bahrain yapata miezi sita iliyopita. Kwa upande mwengine, wananchi wa Iran kesho Ijumaa watafanya maandamano makubwa wakilalamikia unyama na ukatili unaofanywa na wanajeshi wa Bahrain wakisaidiwa na vikosi vya nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi dhidi ya wananchi wa Bahrain.
764163