Rais Ahmadinejad atahudhudria sherehe hizo pamoja na marais wa Tajikistan, Armenia, Iraq, Turkmenistan na Afghanistan.
Wengine wanaohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Zanzibar Seif Ali Iddi, Naibu Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan Omurbek Babanov, Mrithi wa Kiti cha Ufalme Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani , Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Youssef bin Alawi bin Abdullah na Waziri wa Afya wa India Prasanna Acharya na Spika wa Bunge la Pakistan Bi. Fahmida Mirza.
Imearifiwa kuwa viongozi hao watajadili kuhusu kufunguliwa makao makuu ya kudumu ya Nowruz. Aidha watabadilishana mawazo kuhusu ‘Hati ya Nowruz' ambayo itawasilishwa UNESCO na katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Sherehe hizo za siku moja zinalenga kuadhimisha Nowruz kama turathi ya kiutamaduni na kimaanawi ya Iran na nchi zote ambazo husherehekea mwaka mpya wa Kiirani. Machi 21 ilikuwa siku ya kwanza ya mwaka mpya wa 1390 Hijria Shamsia.
766198